Posted on: August 21, 2019 Posted by: Kevin Oduor Comments: 0

Ujenzi wa Thiong’o Wakamilika

Muakilishi wa wadi ya Mountain view Mourice Ochieng amewataka wakaazi wa wadi hiyo kuchukua fursa ya maendeleao eneo hilo kujiendeleza kibiashara. Akizungumza na Mtaani redio alipoongoza ukaguzi wa barabara ya Thiongo, Ochieng amelaumu uongozi uliokuwepo awali kwa kushindwa kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo.Muakilishi huyo wa wadi ameiambia Mtaani redio kuwa kilicho salia ni mwana kandarasi kujenga mabomba ya kupasisha maji taka kando mwa barabara hiyo. Pia taa za usalama zimewekwa.…

Posted on: August 20, 2019 Posted by: Kevin Oduor Comments: 0

Seneta wa Nandi Samson Cherargei kushtakiwa kwa matamshi ya uchochezi

Seneta huyo alikamatwa kutoka nyumbani kwake Eldoret na baadaye akaandikisha taarifa kwa maafisa wa polisi. Seneta huyo anadaiwa kutamka matamshi ya chuki alipokuwa katika mazishi ya mwalimu wa zamani Dominic Kiptoo Choge yaliyofanyika kijiji cha Lelwak, O’lessos – Jumatatu, Agosti 19. Cherargei alitakiwa kufika katika Ofisi za Mkurugenzi wa Uchungizi wa Jinai (DCI) kuhusiana na matamshi aliyoyatoa mwishoni mwa juma – Lakini baada ya kukosa kufika polisi alivyotakiwa kufanya, makachero…

Posted on: August 20, 2019 Posted by: Kevin Oduor Comments: 0

Wakaazi wa Dagoretti watoa maoni yao kuhusu Bajeti ya kaunti

Wakaazi wa eneo bunge la dagoreti kusini walijitokeza kwa wingi katika ukumbi wa Waithaka Juma nne hii kupendekeza hoja ambazo wangetaka ziafikiwe na serikali ya jiji la nairobi katika mwaka wa fedha wa elfu mbili kumi na tisa na ishirini. Kwa mujibu wa wakaazi ambao wamejitokeza katika wadi zote tano wamependekeza suala la kuunganishwa na maji ya serikali ya kaunti kando na  kujengwa kwa barabara ya mitaa . Pius Njogu…

Posted on: August 20, 2019 Posted by: Kevin Oduor Comments: 0

Pogba apoteza penalti na kuzamisha United

Matumaini ya Man United ya kutetea ushindi wao dhidi ya Chelsea katika mechi yao ya ufunguzi kwa msimu mpya, ulizimwa siku ya Jumatatu, Agosti 19 usiku, baada ya Wolves kulazimisha droo ya 1-1 ugani Molineux. Ole Gunnar Solskjaer alifanya mabadiliko kadhaa katika kikosi kilichowachabanga Blues ugani Old Trafford, huku mkufunzi huyo raia wa Norway akimtambulisha Daniel James kwenye nafasi ya Andreas Pereira. United walikuwa kwenye mchakato wa kulipiza kisasi dhidi…

Posted on: August 19, 2019 Posted by: Kevin Oduor Comments: 0

Maraga ahimiza majaji kupunguza mrundiko wa kesi

Jaji mkuu David Maraga  amefungua rasmi kongamano la kila mwaka la majaji katika kaunti ya Mombasa.Kongamano hilo la siku nne linalenga kuleta pamoja majaji  kuzungumzia maswala yanayokumba idara ya mahakama .Majaji zaidi ya mia moja na hamsini wamehudhuria kongamano hilo. Akizungumza katika hafla hiyo,  Maraga ametoa wito kwa majaji kukaza kamba kupunguza mrundiko wa kesi kortini. Pia alieleza baadhi ya mikakati waliyoweka kuhakikisha kuwa  ufisadi umekandamizwa katika mahakama za humu…

Posted on: August 19, 2019 Posted by: Kevin Oduor Comments: 0

Kibra kupata Mbunge mpya tarehe 7 Novemba

Kiti cha Ubunge wa Kibra uliwachwa wazi baada ya Mbunge  Ken Okoth kufariki mwezi Julai baada ya kuugua Ugonjwa wa Saratani ya Utumbo. Wakaazi wa Kibra sasa watarejea debeni tarehe saba mwezi Novemba katika uchaguzi mdogo wa kutafuta mridhi wa Okoth. Tume ya Uchaguzi nchini IEBC imetoa tangazo hilo siku chache baada ya Spika wa Bunge la Kitaifa Justin Muturi kutoa notisi kwenye Gazeti rasmi la serikali Jumatano, Agosti 14 na…

Posted on: August 19, 2019 Posted by: Kevin Oduor Comments: 0

Rais Uhuru Kenyatta aongoza wakenya kuomboleza Msanii wa Benga De’Mathew

Mwandishi: Kevin Oduor Rais Uhuru Kenyatta, Raila na Ruto wameongoza wakenya kuomboleza kifa cha mwanamuziki mashuhuri John De’Mathew  aliyefariki Jumapili, Agosti 18, kwenye ajali ya barabara katika barabara kuu ya Thika kuelekea Kenol. De’Mathew, ambaye alitawala kimziki eneo hilo, alihusika kwenye ajali mbaya kwenye barabara ya Thika karibu na mkahawa wa Blue. Kamanda wa polisi Thika Elena Wamuyu alisema gari la mwanamziki huyo liligonga lorry alipokuwa akitoka kwenye hafla ya Harambee…