Kiti cha Ubunge wa Kibra uliwachwa wazi baada ya Mbunge Ken Okoth kufariki mwezi Julai baada ya kuugua Ugonjwa wa Saratani ya Utumbo. Wakaazi wa Kibra sasa watarejea debeni tarehe saba mwezi Novemba katika uchaguzi mdogo wa kutafuta mridhi wa Okoth. Tume ya Uchaguzi nchini IEBC imetoa tangazo hilo siku chache baada ya Spika wa Bunge la Kitaifa Justin Muturi kutoa notisi kwenye Gazeti rasmi la serikali Jumatano, Agosti 14 na kutangaza nafasi hiyo rasmi kuwa wazi. Nafasi hiyo imekuwa ikivutia wagombeaji wengi ikijumuisha aliyekuwa Seneta mteule Elizabeth Ongoro , Bw Imran Okoth (kaka yake marehemu), Bw Eliud Owalo na aliyekuwa mbunge wa Embakasi Kusini Irshad Sumra.
Tangazi hii sasa itapisha rasmi miezi tatu ya kampeni katika mtaa huo wa mabanda wa Kibera. Chama cha Jubilee hata hivyo haijatangaza nia ya kuwasilisha mwaniaje yeyote kuuridhi nafasi hiyo.
Mwandishi; Kevin Oduor