Jaji mkuu David Maraga amefungua rasmi kongamano la kila mwaka la majaji katika kaunti ya Mombasa.Kongamano hilo la siku nne linalenga kuleta pamoja majaji kuzungumzia maswala yanayokumba idara ya mahakama .Majaji zaidi ya mia moja na hamsini wamehudhuria kongamano hilo.
Akizungumza katika hafla hiyo, Maraga ametoa wito kwa majaji kukaza kamba kupunguza mrundiko wa kesi kortini. Pia alieleza baadhi ya mikakati waliyoweka kuhakikisha kuwa ufisadi umekandamizwa katika mahakama za humu nchini ili kuboresha haki. Baadhi ya malengo ya mahakama ni kuleta haki na usawa katika jamii,uwajibikaji kando na kuhakikisha sheria inafuatiliwa ipasavyo. Baadhi ya mambo ambayo wanatarajiwa kuzungumziwa ni, utendakazi wa majaji na usawa katika jamii.
Mwandishi; Dicosta Kawira