Posted on: August 19, 2019 Posted by: Kamadi Amata Comments: 0

Mwandishi: Kevin Oduor

Rais Uhuru Kenyatta, Raila na Ruto wameongoza wakenya kuomboleza kifa cha mwanamuziki mashuhuri John De’Mathew  aliyefariki Jumapili, Agosti 18, kwenye ajali ya barabara katika barabara kuu ya Thika kuelekea Kenol. De’Mathew, ambaye alitawala kimziki eneo hilo, alihusika kwenye ajali mbaya kwenye barabara ya Thika karibu na mkahawa wa Blue. Kamanda wa polisi Thika Elena Wamuyu alisema gari la mwanamziki huyo liligonga lorry alipokuwa akitoka kwenye hafla ya Harambee ya mwanamziki mwenzake. Viongozi wa eneo la Mlima Kenya wametuma rambirambi zao kwa familia ya De’Mathew ambaye anajulikana sana kwa vibao vyake kama vile ‘Wee ni we njata yakwa’

Mbunge wa GAtundu Moses Kuria alisema mwanamziki huyo hakuwa tu msanii wa kutumbuiza watu mbali nabii ambaye aliotea jamii ya Wakikuyu kuhusu yatakayoikumba. Gavana wa Nairobi Mike Sonko alimsifia De’Mathew kama mmoja wa wanamziki waliokuwa bora zaidi humu nchini. “Ajali ya barabarani imechukua maisha ya mwanamziki aliyekuwa bora wakati wetu, John De’Mathew,” Gavana Sonko aslisema.