Matumaini ya Man United ya kutetea ushindi wao dhidi ya Chelsea katika mechi yao ya ufunguzi kwa msimu mpya, ulizimwa siku ya Jumatatu, Agosti 19 usiku, baada ya Wolves kulazimisha droo ya 1-1 ugani Molineux. Ole Gunnar Solskjaer alifanya mabadiliko kadhaa katika kikosi kilichowachabanga Blues ugani Old Trafford, huku mkufunzi huyo raia wa Norway akimtambulisha Daniel James kwenye nafasi ya Andreas Pereira.
United walikuwa kwenye mchakato wa kulipiza kisasi dhidi ya Wolves ambapo waliwacharaza mara mbili msimu uliyopita. Lakini nia yao ilizimwa, huku wenyeji wakiwa wameimarisha safu yao ya ulinzi ambayo ilifunga mianya yote ya United kuweza kupenya. Hata hivyo, katika kipindi cha kwanza cha mechi hiyo, Mashetani Wekundu walikuwa wamechukuwa udhiti wa mchezo, huku Wolves wakishindwa kuonja wavu.
Mwandishi: Kevin Oduor