Posted on: August 20, 2019 Posted by: Kamadi Amata Comments: 0

Seneta huyo alikamatwa kutoka nyumbani kwake Eldoret na baadaye akaandikisha taarifa kwa maafisa wa polisi. Seneta huyo anadaiwa kutamka matamshi ya chuki alipokuwa katika mazishi ya mwalimu wa zamani Dominic Kiptoo Choge yaliyofanyika kijiji cha Lelwak, O’lessos – Jumatatu, Agosti 19.

Cherargei alitakiwa kufika katika Ofisi za Mkurugenzi wa Uchungizi wa Jinai (DCI) kuhusiana na matamshi aliyoyatoa mwishoni mwa juma – Lakini baada ya kukosa kufika polisi alivyotakiwa kufanya, makachero wameripotiwa kupiga kambi nje ya nyumba seneta huyo mjini Nandi. Maafisa wa polisi walizingira boma la Seneta huyo aliyetarajiwa kujisalimisha  katika Ofisi za Mkurugenzi wa Uchungizi wa Jinai (DCI) kuhusiana na matamshi aliyoyatoa mwishoni mwa juma.