Posted on: August 20, 2019 Posted by: Kamadi Amata Comments: 0

Wakaazi wa eneo bunge la dagoreti kusini walijitokeza kwa wingi katika ukumbi wa Waithaka Juma nne hii kupendekeza hoja ambazo wangetaka ziafikiwe na serikali ya jiji la nairobi katika mwaka wa fedha wa elfu mbili kumi na tisa na ishirini. Kwa mujibu wa wakaazi ambao wamejitokeza katika wadi zote tano wamependekeza suala la kuunganishwa na maji ya serikali ya kaunti kando na  kujengwa kwa barabara ya mitaa . Pius Njogu ambaye ni katibu wa muungano wa wamiliki wa ploti  kaunti ndogo ya  dagoreti akieleza matarajio ya shirika hilo amesisitiza haja ya Gavana wa kaunti ya Nairobi Mike Sonko kuipa kipaumbele miradi itakayoboresha maisha ya wakaazi hao.