Huku zoezi la kuhesabu watu nchini almaarufu sensa likitarajiwa kun’goa nanga usiku wa tarehe ishirini na nne Agosti, wakenya wameonekana kuwa na hofu ya usalama wao iwapo zoezi hilo litakuwa salama. Waziri wa usalama wa ndani Fred Matiangi ameamrisha wamiliki wa vyumba vya burudani kufunga biashara zao mapema ili kupisha shughuli hiyo ya kitaifa. Matiangi ametoa kauli hii katika hafla ya spoti iliyoandaliwa na wizara ya maji katika kaunti ya Meru. Polisi wamejitokeza na kuwahakikishia wananchi usalama wao na kuelezea kuwa mipangilio ipo imara kuimarisha usalama. Vilevile, machifu wa maeneo watahusishwa kwenye zoezi hilo ili kuhakikisha mipangilio hii inatekelezwa.Zoezi hilo kwa mara ya kwanza itatekelezwa kwa njia ya kidijitali nchini.
Na Loise Wambua