Muakilishi wa wadi ya Mountain view Mourice Ochieng amewataka wakaazi wa wadi hiyo kuchukua fursa ya maendeleao eneo hilo kujiendeleza kibiashara. Akizungumza na Mtaani redio alipoongoza ukaguzi wa barabara ya Thiongo, Ochieng amelaumu uongozi uliokuwepo awali kwa kushindwa kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo.Muakilishi huyo wa wadi ameiambia Mtaani redio kuwa kilicho salia ni mwana kandarasi kujenga mabomba ya kupasisha maji taka kando mwa barabara hiyo. Pia taa za usalama zimewekwa.
Na Kamadi Amata.