Posted on: August 28, 2019 Posted by: Kamadi Amata Comments: 0

Chama cha chungwa kilikwa kimeorodhesha wagombeaji kumi na mmoja kumenyana katika uteuzi wa mwaniaji atakayepeperusha bendera ya chama. Hata hivyo, siku tatu kabla ya wakaazi wa Kibra kuelekea debeni, ODM sasa imetangaza kuwa shughuli hiyo itasitishwa kwa muda. Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na Katibu mkuu Edwin Sifuna, wamelazimika kufanya uamuzi huo baada ya serikali kuu kutoa madai ya upungufu wa maafisa wa usalama kulinda shughuli hiyo kwani, wengi wanasaidia katika zoezi la sensa linaloendelea. Zoezi hilo sasa litafanyika tarehe saba mwezi Septemba.

Hayo yakijiri, mgombeaji wa ANC ambaye alikwa mwanamikakati wa Raila Odinga Eliud Owalo ameweza kutwaliwa tiketi na sasa anaendelea kufanya kampeni ya kuridhi kiti hicho.

Chama cha Jubilee kimetangaza kuwa, wale wote wanaopania kuwania kiti cha ubunge Kibra kupitia chama hicho kuwasilisha majina yao kwa zoezi la uteuzi. Kiti hicho kiliwachwa wazi baada ya Mbunge Ken Okoth kuaga dunia baada ya kuugua Saratani ya Utumbo mwezi Julai.