Saturday, December 9, 2023
HomeNewsAfisa wa Polisi auwawa baada ya kuzozana na wenzake Kawangware

Afisa wa Polisi auwawa baada ya kuzozana na wenzake Kawangware

Afisa huyo wa polisi anayetambulika kama Benson Indeche alikwa akihudumu katika kituo cha polisi cha Riruta na alikwa katika ngazi ya Inspekta. Mwendazake anadaiwa kupigwa risasi mara tano mwilini majira ya saa tisa usiku kabla ya kusafirishwa katika hospitali ya Nairobi Women ambapo madaktari walidhibitisha kifo chake.

Inadaiwa kuwa wahudumu wa bodaboda waliripoti kuhangaishwa na polisi huyo ambaye alikwa mlevi. Polisi wenzake walifika pale kun’gamua yaliyojiri. Hata hivyo inadaiwa kuwa mwenda zake alitoa bastola yake na kufyatua risasi. Polisi wamedhibitisha kuwa walimpata na risasi saba mfukoni. Mwili wake ulipelekwa katika hifadhi ya maiti ya Chiromo.

Mwandishi: Kevin Oduor

Kamadi Amatahttps://mtaaniradio.or.ke
I am a digital content creator with niche in Health, politics, and Human Interest Features.
RELATED ARTICLES

Most Popular

Recent Comments

Education Template

Facebook