Posted on: September 23, 2019 Posted by: Kamadi Amata Comments: 1

Wanafunzi 7 wamedhibitishwa kufariki kwenye mkasa wa ukuta kuporomoka na hatimaye madarasa kuanguka katika Shule ya Precious Talent, eneo la Ng’ando, mtaani Dagoretti, jijini Nairobi.

Shule hiyo ipo katika mkabala na Barabara ya Ngong’; shughuli za uokozi zilikamilika huku ikiarifwa tayari wanafunzi zaidi ya 50 wametolewa kwenye vifusi na kupelekwa Hospitali Kuu ya Kitaifa ya Kenyatta (KNH) wanapoendelea kupokea matibabu.

Rais Uhuru Kenyatta, naibu wake William Ruto na kinara wa ODM wameongoza wakenya kuomboleza watoto walioangamia wakisistiza kuwa uchunguzi utafanywa kwa kina kun’gamua chanzo cha mkasa huo.

Aidha waziri wa usalama wa ndani George Magoha aliyefika hapo muda mfupi baada ya mkasa ametangaza wanafunzi waliobaki watasalia nyumbani kwa siku nne ambapo serikali itatoa mwelekeo. Shule hiyo ilikwa na wanafunzunzi 870 huku pia ikidhihirika kuwa hakuna shule ya msingi umma katika wadi hiyo.

Mwandishi: Kevin Oduor