Posted on: September 23, 2019 Posted by: Kamadi Amata Comments: 0

Mwandishi : Fridah Okachi

Mtu mmoja kati ya kumi hupoteza maisha huku watu wawili kati ya kumi wakilazwa kwenye hospitali kutokana na maradhi ya mshtuko wa moyo ulimwenguni. Ripoti hii ikiashiria kuwa idadi ya wanaopoteza maisha kutokana na maradhi ya moyo ni kadri milioni sita kila mwaka kote ulimweguni.
Radhika Choksey msimamizi wa Mawasiliano Dijitali na mauzo katika kampuni ya Philip ,amesema kuwa kuna dakika kumi za kumwokoa yule ambaye anapatwa na mshtuko wa moyo.


Kampuni ya Philip barani Afrika linapania kufahamisha wakenya dhidi ya kukabiliana na mshtuko wa moyo kwa kutoa zaidI ya vifaa ishirini na tano vitakavyozuia vifo hivi kwa shirika la msalaba mwekundu( Red Cross) katika mashindano ya mbio zinazoendelea kwanzia tarehe 21 hadi 29 mwezi September.
Kwa upande wake daktari Muthoni Ntojira kutoka shirika la msalaba mwekundu amesema kuwa tangu kuanzishwa ushirikiano na kampuni ya philip barani afrika ,idadi ya kuokoa maisha kupitia njia ya simu ambayo haitozwi imeongezeka.
Ulimwegu unatarajia kuadhimisha siku ya maradhi ya moyo tarehe ishirini na tisa mwezi Septemba. Maradhi ya moyo, yanasababishwa na hali ya maisha ya watu ,utumiaji kupita kipimo wa sukari,mafuta na chumvi.