Mwandishi: Fridah Okachi
Wakazi, viongozi wa miungano ya mashirika yasiyo ya kiserikali waadhimisha siku ya amani katika mtaa wa Congo.
Josephine Njeri Njiru kiongozi wa shirika la Dagoretti Community Centre,anasema kuwa ukosefu wa amani unasababisha ukosefu wa kazi na kutatiza biashara. Njiru anasisitiza kuwa mkutano huu ni wa kuhamasisha jamii umuhimu wa usalama.
Kwa upande wake Dicksoni Musembi Kasole ambaye ni afisa wa kutoa mafunzo kwa shirika la maendeleo kwa jamii, anasema kuwa kuadhimisha siku ya amani ni jambo ambalo wamekuwa wakilifanya kwa kuhusisha vijana kupata mafunzo yatakayowafanya kuwa na kazi.
Kaunti ya Nairobi imeweza kuandaa sherehe ya kuadhimisha amani huku ulimwegu ukijiunga kuadhimisha siku ya amani tarehe ishirini na mosi mwezi septemba kila mwaka.