Wakurugenzi wa shule ya Precious Talent ilioko eneo la Ng’ando Dagoretti hapa Nairobi wanahojiwa na DCI katika kituo cha polisi cha Kabete. Hii ni baada ya Jumla ya wanafunzi saba kufariki baada ya darasa moja kuporomoka hapo jana.
Miongoni mwa waliofariki kwenye mkasa wa shule ya Precious Talent ni mwanafunzi wa darasa la nane aliyetarajiwa kuufanya mtihani wa kitaifa KCPE.
Lakini mmiliki wa shule hiyo Moses wainaina anailaumu serikali ya kaunti ya Nairobi kwa utepetevu akisema hatua yake kujenga njia ya kupitisha maji taka kando tu mwa shule hiyo imechangia kuporomoka kwake.