Mawingu ya simanzi itagubisha uwanja wa Posta eneo la Ngando huku wazazi na wanafunzi wakitarajiwa kuhudhuria ibada ya watoto 8 waliofariki katika mkasa wa kuporomoka kwa madarasa shuleni humo. Viongozi humu nchini wameendelea kukashifu kifo cha wanafunzi hao huku Serikali ya kaunti ya Nairobi ikiendelea kupokea lalama zaidi. Hatua kadha zimechukuliwa huku Gavana wa kaunti akiwapiga kalamu maafisa 16 wa kaunti kwa kile alichokitaja kama utepetevu kutekeleza majukumu yao.
Soma taarifa hii pia https://mtaaniradio.or.ke/2019/09/23/mashirika-yasiyo-ya-kiserikali-wadi-ya-gatina-kwa-ushirikiano-na-wakaazi-washerehekea-siku-ya-amani-duniani/
Waziri wa elimu George Magoha kwa upande wake alikita kambi katika mtaa wa Kibra. Waziri huyo alifunga shule ya msingi ya St Catherine Bombolulu akihoji kuwa majengo hayo yalikwa na dosari na kutahadharisha maisha ya wanafunzi .Shule zingine 200 zimepewa ilani ya kufunga virago. “Usingoje nikuje ndio mahali , kama uko na majumba kama haya” Mogoha alisema.
Taarifa sawia na hii https://mtaaniradio.or.ke/2019/09/23/dagoretti-wanafunzi-7-waaga-dunia-baada-ya-madarasa-kuporomoka-mtaani-ngando/
Mmilikiwa shule hiyo na wazazi ambao wanao walipoteza maisha wameandikisha taarifa katika kituo cha polisi cha Kabete huku uchunguzi ukiendelea. Naibu wa Rais William Ruto ametoa hakikisho kuwa chini ya miezi mitatu serikali itajenga shule ya msingi katika wadi hiyo.
Mwandishi: Kevin Oduor