Rais Uhuru Kenyatta alimpigia simu mkiambiaji mashuhuri Eliud Kipchoge kumtia moyo huku mwariadha huyo akijitayarisha kwa mbio za INEOS. Kwa video zinazosambaa katika mtandao wa kijamii, rais anaskika akimwmbia Kipchoge kuwa atafaulu.
“Utaweza ndigu yangu na kutoa fahari kwa dunia nzima na vijana kuwa kila kitu inawezekana” Rais alisema akionekana mtu mchangamfu.
Kiongozi wa taifa alichukua nafasi hiyo muda mfupi kabla ya kuelekea katika shule yake ya zamani ya St Mary’s alikosomea kwa hafla ya makumbusho.
Kipchoge anatarajiwa kuvunja rekodi yake ya kukimbia kilomita 42 chini ya masaa mawili na kushikilia rekodi hiyo aliyoiweka katika mbio za Berlin Marathon mwaka wa 2018. Mbio hiyo ina kauli mbiu ya kutoa motisha kwa vijana na watu duniani kuwa hakuna kingingiti chochote kutimiza ndoto ya binadamu.
Iwapo atafanikiwa, atakwa mwanariadha wa kwanza kuwahi kupata ufanisi huo. Mbio hizo zitaanza majira ya saa 9.15 Jumamosi hii mjini Vienna katika taifa la Australia.