Peter Karanja mmoja wa mshukiwa katika mauaji ya bwenyenye Tob Cohen amekamatwa mapema hivi leo nje ya mahakama za Milimani. Mshukiwa huyo amekamatwa kufuatia ilani ya mahakama moja mjini Naivasha.
Mahakama hiyo ilikwa inamsaka Karanja, kwa tuhuma za wizi wa kimabavu. Karanja na Sara Wairimu Kamotho wameshtakiwa na mauaji ya mwanabiashara Mholanzi Tob Cohen. Kukamatwa kwa Karanja kunajiri saa chache baada ya mahakama kuu kuziunganisha kesi ya washukiwa hao wawili, ambapo watalazimika kushtakiwa upya.