Posted on: November 15, 2019 Posted by: Kamadi Amata Comments: 0

Maina Kamanda na gavana wa Kirinyaga Ann Waiguru wameteuliwa kuliongoza hamasisho kuhusu BBI katika eneo pana la mlima Kenya. Hii inafuatia mkutano ambao umeandaliwa katika ikulu ya Sagana na kuhudhuriwa na rais Uhuru Kenyatta. Mkutano huo uliwaleta pamoja viongozi kutoka uliokuwa mkoa wa kati. Kamati hiyo ya kuuza sera iliyomo ndani ya ripoti ya BBI ina wanachama kumi na mmoja. Kando na Waiguru na Kamanda wanachama wengine ni pamoja na Jamleck Kamau kutoka Muranga, Kabando wa Kabando, gavana Francis Kimemia wa Nyandarua, mwenzake wa Nakuru Lee Kinyanjui, Wachira karani kutoka Laikia, Maoke Maore wa Meru, seneta Njeru Ndwiga wa Embu na Petkay Miriti kutoka Tharaka Nithi. Mbunge muakilishi wa kaunti ya Kiambu Gathoni wa Muchomba atakuwa naibu mwenyekiti wa kamati hii itakayoongozwa na Maina Kamanda.