Mwakilishi wa wadi ya Ngando Peter Waihinya amekiri kuwa yuko katika harakati za kufanikisha miradi ya mwaka 2020. Mwakilishi huyo alitoa kauli hii katika mahojiano ya kipekee na mwandishi wetu juma tano hii. Miradi hii ni pamoja na ukarabati wa barabara kadhaa eneo hilo kando na usambazaji wa maji kwa wakaazi wa eneo hilo. Kumbuka eneo hilo la Ngando linachangamoto si haba. Wazazi wanalazimika kupeleka wanao kwa shule za kibinafsi kwani wadi hiyo haina shule na hospitali ya umma.
STL Yamumo