Friday, June 14, 2024
HomeLifeStyleWanabiashara wa Kawangware walilia Ushuru wa Uzalendo 'Patriotism Tax'

Wanabiashara wa Kawangware walilia Ushuru wa Uzalendo ‘Patriotism Tax’

Je ,wafahamu ukiwa mfanyabiashara mdogo ambaye anapata shilingi 1000 utahitajika kulipa ushuru wa uzalendo(patriotism tax)? iwapo una duka la matunda ,sehemu ya kuuzia mboga, duka la ususi almaarufu salon ama biashara yoyote ndogo uwe tayari kuanza kulipa ushuru.

Kwa kila mfanyabiashara ambaye anapata kima cha shilingi elfu moja kwa siku atahitajika kulipa ushuru wa shilingi thelathini kila mwezi kwa mamlaka la kutoza ushuru hapa nchini.Mamlaka ya ukusanyaji ushuru (KRA) ipo kwenye harakati za kutekeleza sheria ya ukusanyaji ushuru yenya utata ya asilimia tatu ya mauzo kila mwezi na hivyo kulenga wafanyabiashara milioni 2.5. Utelekezaji huu ukitarajiwa kuanza tarehe moja mwezi januari mwaka huu.Ushuru huu wa uzalendo hauadhiri utendakazi wa biashara yako.

Mfanyibiashara wa chini atahitajika kuweka rekodi za kudhibitisha kuwa anafuata sheria na wakati wa ukaguzi wa rekodi na shirika la KRA.

Kwa wanao lipa leseni ni vyema kufahamu kuwa atahitajika kulipa zaidi kwa asilimia kumi na tano zaidi hii ikiwa ni shilingi mia saba hamsini kwa wale wanapata leseni ya shilingi elfu tano.Kwa leseni ya shilingi ya elfu kumi utahitajika kulipa shilingi elfu moja na mia tano zaidi. Wafanyabiashara wa salon, maduka ya nyama wakihitajika kuandikisha biashara katika mitandao na kulipia kila mwezi.

Ushuru huu wa uzalendo ukiwaanza waliosajiliwa kwenye ushuru wa vat, wafanyabiashara wanaopata zaidi ya milioni tano kwa mwaka. Shoka hili la utelekezaji wa ushuru wa uzalendo ukitaka wamiliki wa trekta kuhitajika kulipa asilimia kumi na sita ila kwa trekta za kilimo zikiponea shoka.

Je, kwa kampuni za kamari zikipata pigo kwa kutakiwa kulipa asilimia 20.ushuru huu ukiongezwa zaidi ili kupunguza shughuli za kucheza kamari.Uzalendo huu ukiwa afueni kwa wawekezaji wa kutengezeza upya watalazimika kulipa asilimia kumi na tano kwa kipindi cha miaka mitano kinyume na hapo awali walipokuwa wakilipa asilimi 30. Msuada huu uliotiwa sahihi na rais uhuru kenyatta ukijitenga na aina yeyote ya dhamana itakayo tumika katika miradi au miundo misingi ikikosa kutozwa.

 Hata hivyo muungano wa kutetea maslahi ya mfanyikazi ikienda mahakamani kupinga ushuru huo  na kutaka serikali kuangalia upya njia mwafaka ya kutoza ushuru kwa mfanyabiashara mdogo. muungano huo wa cuto ukisema kuwa itayumbisha uchumi wa taifa na kusababisha ukosefu wa ajira kwa wakenya.

Kamadi Amata
Kamadi Amatahttps://mtaaniradio.or.ke
I am a digital content creator with niche in Health, politics, and Human Interest Features.
RELATED ARTICLES

Most Popular

Recent Comments

Solverwp- WordPress Theme and Plugin

Facebook

adapazarı escort Eskişehir escort bayan