Huku shule zikifunguliwa kwa muhula wa kwanza, baadhi ya shule nchini wanapitia changamoto za kuendesha masomo yao kama kawaida. Mojawapo ya changamoto hizi ni ukosefu wa vitabu, walimu tosha na hata vyakula.Eneo la Kabiria Dagoretti, watoto wa shule ya msingi ya Kangaroo Junior School wamelazimika kusalia nyumbani kwani,shule haina uwezo wa kuwalisha.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo Truphesa Ondiso anasema kuwa ndoto ya wanafunzi hao imekwama kwani mhisani aliyekuwa anatoa usaidizi wa vyakula alisitisha. Hata hivyo shule hiyo inataka wazazi kuwachilia wanao 150 kurejea shuleni licha ya changamoto hizi. Mkuu huyo wa shule anatoa wito kwa wasamaria wema kujitokeza na kufadhili mradi huo wa chakula shuleni.
Mwandishi : Fridah Okachi