Jaji John Mativo alitoa amri hii Ijumaa akiskiza kesi iliyokuwa unaangazia uwezekano wa wakili Miguna Miguna kurejea nchini. Mativo anasikitika na mienendo ya serikali kukaidi amri za mahakama zilizotolewa mwaka wa 2018 Miguna alipofurushwa kuelekea Canada kwa lazima.
Wakili Christopher Marwa aliyewasilisha serikali kwa mara ya kwanza kuhusu kesi hiyo anasema kuwa Paspoti ya kusafiri yenye Miguna anayo ni ya zamani na kumkubalia kutua kinyume bila stakabadhi tajika ni kukiuka sheria za kimataifa ya kusafiri.
Juma tatu wiki Jaji Weldom Korir aliamrisha Serikali kurejesha Miguna nchini bila shinikizo yoyote. Mativo ametoa amri kwa Mwanasheria wa serikali Kihara Kariuki kufika mahakamani Juma tatu wiki ijayo kuelezea msimamo wa serikali kuhusu masaibu ya Miguna.
Mwandisi: Michael Barnabe