Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria alipongeza Rais Uhuru Kenyatta kwa kufanya mabadiliko kwenye serikali yake. Kuria alikutana na aliyekuwa waziri wa Kilimo Mwangi Kiunjuri na kuashiria huenda wakaanza ushirikiano wa kisiasa.
Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari kabla ya kukutana na Kuria, Kiunjuri alikuwa amewaambia wanahabari kuwa haendi popote alipoulizwa iwapo atakuwa anajiunga na siasa za kitaifa. “Siendi popote … nitakuwa na nyinyi tu huku … Nashukuru Mungu kwani nimekuwa nikipitia hali ngumu. Nilidhalilishwa na ni Mungu pekee na familia yangu ambao wanajua niliyopitia,” alisema Kiunjuri.
Kiunjuri alipigwa kalamu baada ya Rais kufanya mabadiliko katika baraza lake la mawaziri.Monica Juma aliyekuwa katika wizara ya masuala ya nje amepelekwa kwa ulinzi, huku Rachael Omamo aliyekuwa ulinzi akichukua nafasi ya Monica Juma. Seneta wa Nyeri Mutahi Kagwe ametwaliwa Afya huku Peter Munya akipewa nafasi ya ukulima alipotemwa Kiunjuri.
Mwandishi Kevin Oduor