Kwenye kanda ya video iliyosambazwa katika mtandao wa kijamii, jamaa anayeaminika kuwa Babu na ambaye alikuwa amevalia shati lenye rangi ya machungwa alionekana akimfyatulia risasi kadhaa DJ huyo mwendo wa saa moja asubuhi Ijumaa.
Maafisa wa polisi waliweza kumkamata Babu saa chache baada ya kisa hicho na anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Kilimani. Tayari uchunguzi umeanzishwa kuhusiana na kisa hicho huku Babu akida kutishiwa maisha na mahasidi wake wa kisiasa.
Mwandishi : Kevin Oduor