Babu alikana mashtaka dhidi yake na atazuiliwa kwa siku saba zaidi huku uchunguzi dhidi yake ukiendelea. Kama ilivyoripotiwa awali, Babu alikamatwa baada ya kumpiga risasi na kumjeruhi vibaya DJ huyo siku ya Ijumaa, Januari 17.
Wakili wa Owino Cliff Ombeta alitaka mteja wake aachiliwa huru kwa dhamana ila hakimu mkuu wa mahakama ya Milimani Francis Andayi alikataa ombi hilo kwa madai kuwa mshukiwa angeharibu ushahidi. Babu kwa sasa anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Gigiri huku DJ Evolve akiendelea kupokea matibabu katika hospitali ya Nairobi. DJ Evolve anatarajiwa kufanyiwa upasuaji 3 kulingana na ripoti ya daktari.
Ripoti ya Kevin Oduor