Mwili wa msichana wa umri wa miaka kati ya kumi na minaNe na ishirini na sita ulipatikana kwenye mto karibu na eneo la Cabby Centre Kabiria. Msichana huyo anaaminika kuwa alikuwa ameuwawa na kufungwa na kamba kisha kuwekwa kwenya gunia na mwili wake kutupwa kwenye mto. Baadhi ya wakaazi waliopata mwili huo wanahoji kuwa walipoenda kuteka maji katika Kisima kilichokaribu, waliskia harufu wa na kufika hapo walipopata mwili huo. Mwili ulipelekwa katika hifadhi ya Maiti ya City huku Polisi wakiendeleza uchunguzi.
Mwandishi : Delphine Maita