Wabunge wa Jubilee wakiongozwa na Seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen wametangaza amza hiyo. Kiongozi huyo aliyetoa hotuba kwa wanahabari pamoja na Alice Wahome, Moses Kuria, Aisha Jumwa na wengine wamesema kuwa wataalika viongozi wote nchini kutoa maoni yao kando la kupeleka nakala kwa wananchi.
Seneta Kipchumba Murkomen alizua hisia mseto Jumamosi, Januari 25, baada ya kugeuka ghafla na kuanza kumsifia kinara wa ODM Raila Odinga. Kando na kumsifu Raila kwenye jukwaa alipopewa kipaza sauti, picha zinaonyesha Murkomen akimsalimia kiongozi huyo wa ODM kwa heshima kubwa.
Murkomen anatoa kofia kama ishara ya heshima na kisha kupinda kiuno na kumpa Raila mkono wake tayari kwa salamu. Hiyo huyo ni ishara ya heshima kuu kwa kiongozi na huonyesha kuwa mtu anamtambua vilivyo. Hilo halikutarajiwa kwa mwandani huyo wa Naibu Rais ambaye awali amekuwa akitoa cheche za maneno dhidi ya Raila.