Posted on: February 4, 2020 Posted by: Kamadi Amata Comments: 0

Rais Mstaafu Daniel arap Moi afariki dunia akiwa na miaka 95, rais Uhuru Kenyatta athibitisha.

“Kwa masikitiko makubwa natangaza kifo cha kiongozi mkubwa Afrika, Daniel Toroitich arap Moi, rais wa pili wa Kenya. Raisi mstaafu amefariki katika Hospitali ya Nairobi mapema asubuhi ya leo Februari 4 akiwa na familia yake.

Msemaji wa Mzee Moi Lee Njiru, amesema mipango yote ya mazishi ipo chini ya jeshi la Kenya kwa kuwa Mzee Moi alikuwa amiri jeshi mstaafu wa nchi.

Mzee Moi alizaliwa Septemba 2, 1924 na alitawala Kenya kwa miaka 24 kutoka 1978 mpaka 2002.