Mwandishi: Kevin Oduor
Kupitia kwa Mkuu wa Utumishi wa Umma Joseph Kinyua, serikali pia imetoa utaratibu utakaofuatwa wakati wa shughuli ya mazishi hadi atakapozikwa mzee. Moi aliyeaga dunia Jumanne, 4 akipokea matibabu katika Nairobi Hospital atazikwa Jumanne, nyumbani kwake Kabarak, Kaunti ya Nakuru.
Rais Uhuru Kenyatta ataongoza wakenya kutizama mwili wa RaiS Moi katika bunge la taifa siku ya Jumamosi. Ibada ya wafu itaandaliwa Juma Nne kabla ya mwili kupelekwa nyumbani kwake Nakuru atakapozikwa.