Posted on: February 6, 2020 Posted by: Kamadi Amata Comments: 0

Visa vya utovu wa usalama vimeendelea kushuhudiwa Kaunti ndogo ya Dagoretti. Alhamisi asubuhi, mwili wa mwanaume ulipatikana umetupwa kando ya barabara ya Ndwaru. Wale waliyoshuhudia mwili huo, wameiambia Mtaani radio, kuwa mwili huo ulipatikana majira ya saa kumi na mbili alfajiri.Hadi tukienda hewani haukuwa umetambuliwa huku wenyeji wakihoji kuwa huenda akauwawa kwingine na kisha mwili wake kutupwa hapo. Mwili huo umepelekwa katika hifadhi ya maiti ya city.