By Kevin Oduor
Polisi huyo ambaye anaaminika kuwa alikwa na taarifa muhimu kuhusu sakata ya zabuni ya kununua vifaa vya jeshi alipatikana chumbani kwake wiki iliyopita akiwa amefariki. Kulingana na upasuaji uliofanywa na serikali, sajini huyo alikwa na donda moja la risasi chumbani.
Sajini Kenei alionekana mara ya mwisho akiwa na maafisa wenzake aliokuwa akihudumu nao katika afisi ya Ruto – Kenei alipatikana akiwa ameaga dunia nyumbani kwake mtaani Imara Daima Alhamisi.
Alitarajiwa kuandikisha taarifa katika makao makuu ya DCI kuhusu sakata ya KSh 40 bilioni inayomkabili aliyekuwa waziri wa michezo Rashid Echesa – Ripoti za awali ziliarifu kuwa Kenei huenda alijitoa uhai lakini familia imepinga vikali madai hayo.
Maafisa wa upelelezi wanaendelea kufanya uchunguzi kubaini kilichosababisha kifo cha Sajini Kipyegon Kenei ambaye alikuwa akihudumu katika afisi ya Naibu Rais William Ruto ya Harambee Annex. Kenei alipatikana akiwa ameaga dunia nyumbani kwake mtaani Imara Daima.