Saturday, April 20, 2024
HomeNewsKutana Na Msanii Mwalimu Zilla Kutoka Hapa Dagoreti!

Kutana Na Msanii Mwalimu Zilla Kutoka Hapa Dagoreti!

Na Changez Ndzai

Msanii wa  Nyimbo za Injili Mwalimu Zilla

Ni mmoja kati ya wasanii wachanga wanao jituma kupitia mziki, Zilla anafanya mziki wa injili na amekua akitumia kipaji cha ususani ili kueneza injili. Godfrey Wekesa ama kwa jina la msimbo Mwalimu Zilla, anasema mziki kwake ndio njia ya kujipatia kipato. Akiwa anavibao kadhaa ambavyo amerekodi na tena ameshawahi kuvifanyia video, muimbaji huyu wa Inuka amekua kielelezo chema kwa wasanii wengine ambao wanatamani kuwa kwenye viatu vyake. Akiongea na meza yetu ya habari ya Mtaani Radio, Zilla anasema siri kubwa ya mafanikio yake ni kumweka Mungu mbele, kuwa na heshima na uvumilivu bila kuacha nyuma kutia bidii kwenye kazi yake ya uandishi, kurekodi na kusamabaza kazi zake za mziki.

Mwalimu Zilla, wakati akirekodi video ya mojawapo ya wimbo wake.

Mbali na kutoa kazi zenye kumtukuza mweneyzi Mungu, Zilla pia mwaka huu aliingia studio na kurekodi kibao cha kuwasifu mashujaa wa Kenya. Kwenye kibao hiki alichokipatia jina la “Shujaa’’ ameongelea sana kuhusu matukio ambapo askari wetu nchini Kenya wamekua wakijitoea kuokoa maisha ya wazalendo wakati wa matukio ya kigaida mfano matukio kama yale ya hoteli ya Westgate na hoteli ya kifahari ya Desit, huku bila kuwaacha nyuma mashujuaa wetu na wapiganaji wa vita vya maumau na kadhalika.

Akiongelea kuhusu changamoto na jinsi anavyo kabiliana nazo kwenye mziki, Mwalimu Zilla anasema hatua yote ya utengenezaji wa mziki kuanzia uandishi, kurekodi hadi kutengeneza video huwa ni changamoto kubwa. Maana mziki siku hizi umekua ni biashara, na kama biashara yeyote ile mtu anafaa kua na mtaji wa kumuanzishia bishara. Hivyo kwa upande wake anasema wasanii wengi wenye vipaji wamekua waki wama kwa kukosa mtaji wa kuanzishia kazi zao haswa kuingia studio na kurekodi muziki.

Mwalimu Zilla, akisifu wakati akirekodi video ya mojawapo ya wimbo wake.

Zilla anasema kuwa hata baada ya wasanii kuweza kupata nafasi ya kuingia studio na kurekodi changamoto nyingine inakua ni usambazaji wa mziki huo. Hivyo Mwalimu zila anasema anafurhia kwa Mtaani Radio kupitia vipindi vyake ikiwemo Muzuka na vipindi vingine kwa kutengenza meza ya kusukuma na kutangaza kazi za wasanii wa Dagoreti kama yeye ambao wanajituma kukimu maisha kupitia mziki. Katika vibao vingine ambavyo ameshawahi kuvitoa ni pamoja na Blessed na Eliud Kipchoge ambacho alimtungia mwanariadha huyo wa humu nchini Kenya.

Edited By Kamadi Amata

editor@mtaaniradio.or.ke

Kamadi Amata
Kamadi Amatahttps://mtaaniradio.or.ke
I am a digital content creator with niche in Health, politics, and Human Interest Features.
RELATED ARTICLES

Most Popular

Recent Comments

Solverwp- WordPress Theme and Plugin

Facebook

adapazarı escort Eskişehir escort bayan