Tuesday, June 11, 2024
HomeNewsMtaani Radio Kuboresha Mazingira Dagoreti!

Mtaani Radio Kuboresha Mazingira Dagoreti!

Na Changez Ndzai.

Mkurugenzi wa Mtaani Radio (katikati) Kelvin Nyangweso akiwa katika zoezi la usafishaji

Suala la kuweka mazingira bora katika maeneo tunayoishi haswa maeneo ya kibiashara linafaa kuzingatiwa na kupewa kipao mbele katika jamii. Afya njema ya binadamu hutegemea na mazingira yaliyo safi na dhabiti yanayomuzunguka mwananchi haswa kwa wakazi wa Dagoreti. Kwa sababu hii kituo cha redio cha Mtaani Radio, kilijivika kilemba na kutenga siku ya usafi kila jumamosi ya mwisho ya kila mwezi.

Mashabiki na watangazaji wa Mtaani radio walijumuika pamoja kufanya usafi katika maeneo tofauti ya Dagoreti na vitongoji vyake.

Wakubwa kwa wadogo walijitokeza kudumisha usafi Dagoretti.

Wakiongozwa na mkurugenzi wa Mtaani Radio,Kelvin  Nyangweso na nahodha wa kipindi cha Oya Oya Michael Barnabe, wananchi ambao wengi pia walikua ni mashabiki wa Mtaani radio, waliweza kusafisha maeneo ya Kabiria baada ya kukutana katika makao makuu ya Mtaani radio yaliyopo kwenye majengo ya Kivuli Centre.

Shughuli hii ilianza katika Shule ya msingi ya Kabiria, shughuli hiyo ilifuata mkururu na kuelekea hadi mtaa wa Satellite na kufikia kikomo katika eneo la Kwa Maji. Akioongea kwa kina kuhusu mradi huu wa kutunza mazingira hapa Dagoreti, nahodha wa kipindi cha OyaOya  Michael Barnabe, anasema uendelezi wa shughuli nzima ya kusafisha ama kuboresha mazingira ndani ya Dagoreti utakua unafanyika mara kwa mara ili kuwapa hamasa wananchi na kuona umuhimu wa kuishi kwenye mazingira bora kwa afya njema na bora.

Mtangazaji wa kipindi cha OyaOya Michael Barnabe (Kushoto) akiongoza katika uzoaji taka Kabiria.

Hata hivyo kupitia Mtaani radio, kuna haja ya wananchi wanao ishi maeneo ya Dagoreti kuzingatia na kufata mkondo huu wa kuweka mazingira masafi. Elimu hii ya kuboresha sehemu wanazoishi  binadamu haifai kuishia tu kwa siku maalumu zinazo tengwa na mradi kama huu ulio anzishwa na Mtaani Radio bali wazazi wakiwa nyumbani waweze kupitisha ujumbe kwa watoto wao ama vijana kuhimiza wanarika wenzao jinsi ya kuwa na siku maalumu za kusafisha mitaa yetu ama makazi yetu.

 Sikusafisha tu pekee, bali upanzi wa miche wakati wa mvua ili kukuza miti ambayo nitegemeo  kubwa kwa  binadamu si kwa tu kutupa hewa safi, ila pia miti  ni kivutio kikubwa cha mvua na faida nyinginezo.

Edited by Kamadi Amata

editor@mtaaniradio.or.ke

Kamadi Amata
Kamadi Amatahttps://mtaaniradio.or.ke
I am a digital content creator with niche in Health, politics, and Human Interest Features.
RELATED ARTICLES

Most Popular

Recent Comments

Solverwp- WordPress Theme and Plugin

Facebook