Tuesday, October 15, 2024
HomeNewsMbunge wa Msambweni Suleiman Dori Aaga dunia!

Mbunge wa Msambweni Suleiman Dori Aaga dunia!

Mbunge wa eneo bunge la Musambeni mheshimiwa Suleiman Dori aiaga
dunia. Dori ambaye hadi kifo chake alikua akiwahudumia wananchi wa
Msambweni na amekua mwandani wa karibu wa naibu wa raisi William Samoi
Ruto. Kitu ambacho kimewahi kumletea shida hadi kutaka kutemwa nje ya
chama chake cha ODM pamoja na mheshiwa wa eneo bunge la Malindi
Mheshimiwa Aisha Jumwa. Hata hivyo Suleiman kufikia kifo chake amekua
akipokea matibabu katika hospitali ya Aga Khan jijini Mombasa, ambapo
anasemekana amekua akipigania maisha yake kutokana na makali ya
ugonjwa wa saratani ambao hatimae umefanikiwa kuuchukua uhai wake.

Akidhibitisha kifo chake mbunge mwenzake wa eneo bunge jirani la
Kinango Mheshimiwa Benjamin Tayari, amesema ni kweli Dori ameaga dunia
alfajiri ya leo siku ya Jumatatu saa kumi na moja asubuhi. Akiongezea
zaidi msemaji wa familia Bw. Shahame Azizi amesema tayari mwili wa
mwendazake umehamishwa kutoka hospitali ya Aga Khan iliyopo jijini
Mombasa hadi kijijini kwao kule Ghasi katika eneo bunge lake la
Msambweni ambapo utasitiriwa leo majira ya saa kumi jioni kulingana na
taratibu za didni ya kislamu. Dori ameaga dunia akiwa na umri wa miaka
43 na alikua anatumikia wananchi wa Msambwani kwa kipindi chake cha
pili baada ya kukihifadhi kiti hicho kwa mara ya pili kutokana na
kuingia bungeni kwa mara ya kwanza munamo mwaka wa 2013 na
akachaguliwa tena 2017 ambapo amehudumu hadi kifo chake Jumatatu ya
leo.

Viongozi mbalimbali wakisiasa kote nchini wametoa rambirambi zao kwa
wanafamilia, akiwemo naibu wa raisi William Samoe Ruto, ambaye
amemtaja kama mwanasiasa shupavu na mpenda maendeleo, Mheshimiwa spika
wa bunge la kitaifa Justini Mturi amemutaja kama kiongozi jasiri na
mpiganaji wa haki na maendeleo kwa wananchi wake. Huku Gavana wake wa
Kwale Mheshimiwa Salim Mvurya akimtaja kama kiongozi mwenye maonao na
mwelekeo mwema si kwa wananchi wa Msambweni pekee bali kwa Pwani nzima
kwani hadi kifo chake ikumbukwe kuwe alikua katibu mkuu wa chama cha
wabunge wa Pwani (Coastal Parliamentary Group). Kiongozi wa kitaifa wa
chama chake cha ODM Mheshimiwa Raila Odinga na Raisi Uhuru Kenyatta
pia wametoa rambirambi zao kwa wanafamilia na haswa kwa wanachi wake
wa eneo bunge la Msambeni.

Kamadi Amata
Kamadi Amatahttps://mtaaniradio.or.ke
I am a digital content creator with niche in Health, politics, and Human Interest Features.
RELATED ARTICLES

Most Popular

Recent Comments

Solverwp- WordPress Theme and Plugin

Facebook

adapazarı escort Eskişehir escort bayan