Thursday, April 11, 2024
HomeNewsMkenya wa Kenya wa kwanza augua virusi vya Corona

Mkenya wa Kenya wa kwanza augua virusi vya Corona

Mwandishi: Kevin Oduor

Wizara ya Afya imeripoti kisa cha kwanza cha virusi vya ugonjwa wa corana nchini. Kulingana na Waziri wa Afya Mutahi Kagwe, Mkenya huyo alithibitishwa kuwa na virusi hivyo usiku wa Alhamisi, Machi 12 baada ya kurejea nchini kutoka Marekani.

Mgonjwa huyo mwenye umri wa miaka 27, alithiitishwa kuwa na virusi hivyo, Alhamisi, Machi 5 na amelazwa katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta (KNH). Waziri ameripoti kuwa, mgonjwa huyo wa kike aliyejipeleka hospitali mwenyewe baada ya kuhisi maumivu anaendelea vizuri na matibabu, na kwamba joto lake la mwili limepungua.

Pia sekta ya Uchuuzi wa Umma imetakiwa kuchukua tahadhari ya mapema na kuhakikisha inawapa wateja wao sabuni za maji zenye kemikali ya kuua vidudu.

Kufikia sasa, nchi zaidi ya 100 zimeripoti visa vya virusi vya corona huku Kenya ikiwa nchi ya 13 Afrika kuripoti kisa. Duniani kote visa zaidi ya 134,930 vimeriptiwa huku idadi ya walioaga dunia kufuatia mchamko wa virusi hivyo ikifikia 4,990. Waliopona baada ya kunaswa na virusi hivyo ni watu 70,396.

Kamadi Amata
Kamadi Amatahttps://mtaaniradio.or.ke
I am a digital content creator with niche in Health, politics, and Human Interest Features.
RELATED ARTICLES

Most Popular

Recent Comments

Solverwp- WordPress Theme and Plugin

Facebook

adapazarı escort Eskişehir escort bayan