Posted on: March 24, 2020 Posted by: Kamadi Amata Comments: 0

By Kevin Oduor

Kakamega

Wycliffe Oparanya alitangaza kuwa atafanyiwa vipimo vya Covid-19. Hii ni baada ya kutangamana na maafisa watatu ambao walisafiri nchini Italia hii majuzi ambapo ndio imeathiririka zaidi na janga hilo. Watatu hao walikosa kufuata kanuni ya kuingia karantini wiki moja iliyopita baada ya kurejea nyumbani.

Oparanya pia ametambua kwamba maafisa hao watatu hawakujitenga ghafla baada ya kurejea nyumbani wakitokea Italia ambapo walikuwa wamekwenda kutafuta kifaa cha maji kinachohitajika na kaunti hiyo.

Watatu hao huenda wakakamatwa kwa kukiuka maagizo ya serikali ambapo kila mtu anayeingia nchini ni lazima kujitenga kwa siku 14.