Posted on: March 31, 2020 Posted by: Kamadi Amata Comments: 0

Wakaazi wanaoishi maeneo ya kilimani, westlands na kibra wako katika hatari kubwa ya kuambukizwa virusi vya covid 19. Katika ramani inayotumiwa na wizara ya afya kuwatafuta watu waliyotangamana na mmoja wa virisi hivyo inaonyesha kuwa wakaazi wengi wako katika maeneo ya Kilimani, Kibra, Westlands, Makadara, na  Starehe.

Wengine wako katika kaunti ndogo za Kamkunji, (Embakasi East, West, Central, North and South), Roysambu, Langata, Kiambaa, Kajiado North na  Kasarani.

Aidha ni maazi tisa pekee ambayo yametajwa kutokuwa na jamaa aliyekongamana na mtu aliye na virusi vya covid 19. Kaunti hizo ndogo ni pamoja na Ruiru, Mavoko, Kiambu, Kabete, Limuru, Kikuyu, Dagoretti, na Kajiado East.

Jana jumatatu waziri wa afya Mutahi Kagwe alisema kuwa watu hamsini wenye wametangazwa kuwa na virusi hivyo wametangamana na wengine elfu moja mia nne ishirini na sita.