Kenya imethibitisha visa tisa zaidi vya wajonjwa wa covid-19. Waziri msaidizi wa afya Daktari Mercy Mwangangi amesema tisa hao ni kati ya waliyopimwa kwa saa ishirini nan ne zilizopita.Tisa hao sasa wanafikisha idadi ya wakenya ambao wameambukizwa virusi hivyo kufikia hamsini na tisa.
Daktari mwangangi amesema kwa kipindi cha saa ishirini na nne zilizopita watu mia mbili thelathini na wanne wamepimwa. Tisa kati yao wamepatikana na virusi hivyo.
Aidha amesema serikali inawafuatilia watu elfu moja mia moja na sitini ambao walikongamana na wale ambao wamepatikana na virusi hivyo.
Serikali ilikataa kuchukua maswali kutoka kwa waandishi wa habari na kushikilia kuwa hilo litaendelea hadi hapo kesho.