Waziri wa Afya Mutahi Kagwe
Idadi ya watu walioambukizwa virusi vya corona nchini imetimia 110, waziri wa Afya Mutahi Kagwe ametangaza. Akizungumza katika mkutano na wanahabari Alhamisi hii, Kagwe alisema kuwa watu wengine wawili wamepoteza maisha yao kutokana na maambukizi ya virusi hivyo.
Hivyo basi idadi ya waliofariki kutokana na virusi hivyo nchini imefikia watatu. Kagwe pia amepiga marufuku safari za kuelekea mashambani akionya Wakenya kwamba huenda wakaeneza maambukizi ya virusi hivyo kwa kiwango kikubwa.
Waziri Kagwe pia amechukua nafasi hiyo kuwaponda wakenya wanaokejeli wakenya wawili Brenda na Brian waliotangazwa kuwa walipona virusi hivyo.