Monday, September 25, 2023
HomeNewsCOVID 19 UpdatesCornona-Idadi yafikia 122

Cornona-Idadi yafikia 122

Idadi ya wagonjwa wa virusi vya corona nchini imefikia watu 122. Hii ni baada ya watu wengine 12 kuthibitishwa kuwa na virusi hivyo ndani ya saa 24 zilizopita.

Waziri msaidizi katika wizara ya Afya Daktari Mercy Mwangangi,amesema kwamba kati ya raia hao waliopatikana na virusi hivyo ni Wakenya 11 na raia mmoja wa Somalia.

Wakati huo uo Kenya imepoteza mgonjwa mwengine kupitia virusi hivyo na kufanya idadi ya waliofariki kufikia watu 4.

Mgonjwa huyo ni mvulana wa miaka sita ambaye alikuwa akiugua ugonjwa uliokuwa ukiathiri kinga yake.

Maafisa wa afya waliokuwa wakimhudumia mvulana huyo katika hospitali kuu ya kitaifa ya Kenyatta wamewekwa karantini. Madaktari waligundua mtoto huyo alikuwa na virusi hivyo baada ya kifo chake.

Kamadi Amatahttps://mtaaniradio.or.ke
I am a digital content creator with niche in Health, politics, and Human Interest Features.
RELATED ARTICLES

Most Popular

Recent Comments

Education Template

Facebook