Waziri wa Afya Mutahi Kagwe ametangaza watu wanane zaidi wameambukizwa virusi vya corona nchini. Wakati Huo uo ametangaza kulegeza masharti kwenye hoteli inayouza chakula.
Tangu mara ya kwanza kisa cha ugonjwa huo ulipotangazwa nchini, idadi ya waliyoambukizwa imefikia 363.
Wagonjwa 8 pia wamethibitishwa kupona na kufikisha jumla ya idadi hiyo kuwa 114.
Wote walioambukizwa hawana historia ya kusafiri nje ya nchi.Hatua hii inamaanisha kuwa bado kuna maambukizi ya Ndani kwa ndani.
Wizara ya afya pia imesema kuwa itaruhusu hoteli kuanza kufunguliwa kuanzia saa kumi na moja alfajiri hadi saa kumi jioni. Huduma ya wateja kujipakulia chakula imeondolewa. Aidha wale watakaoruhusiwa kupakua chakula ni wale watakaokuwa wamepimwa.