Posted on: April 28, 2020 Posted by: Kevin Oduor Comments: 0

Wakaazi wanne wa Kawangware ni miongoni mwa wagonjwa kumi na moja waliyoambukizwa virusi vya Covid-19. Katibu wa kudumu katika wizara ya afya Rashid Aman, amesema Taifa sasa liko na wagonjwa 374. Umri wa wale waliyoambukizwa ni kati ya miaka mitatu na sabini na tano.

Nairobi ina visa 7 huku Mombasa ikiwa na visa 4. Wagonjwa wote wa Mombasa wanatoka eneo la Kibokoni.

Watu 589 walipimwa katika muda wa saa 24 zilizopita.

Watu wengine 10 wamepona virusi hivyo vya Covid-19 na kufikisha idadi ya waliopona kufikia 124.

Kaunti za Nairobi na Mombasa zimechangia asilimia tisini ya wagonjwa hao.

Wakati huo uo Katibu huyo wa kudumu katika wizara ya afya, amesisitiza kuwa kufunguliwa kwa Migahawa sio kufunguliwa kwa sehemu za burudani.