Posted on: June 22, 2020 Posted by: Kevin Oduor Comments: 0

Aden Duale sio kiongozi wa wengi tena katika bunge la kitaifa. Hii ni baada ya chama chake ya Jubilee kumvua wadhifa huo. Duale amehudumu katika nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka minane sasa.

https://www.youtube.com/watch?v=nMLVB-_j_tU&feature=youtu.be

Mbunge wa Kipipiri na waziri wa zamani Amos Kimunya ndio sasa kiongozi wa wengi. Hii inafuatia mkutano wa wabunge wa chama cha Jubilee ulioongozwa na rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto. Mkutano huu uliandaliwa katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa ya KICC.

Aidha katika mabadiliko haya mapya, muturi kigana sasa ndiye mwenyekiti wa kamati ya bunge kuhusu haki, sharia na haki za kibinadamu. Mbunge wa kieni kanini kega ndiye mwenyekiti wa kamati ya bunge kuhusu bajeti.