Posted on: July 6, 2020 Posted by: Kevin Oduor Comments: 0

Rais Uhuru Kenyatta ametangaza kuwa mipaka ya kaunti ya Nairobi, Mombasa na Mandera zitafunguliwa rasmi Jumanne Julai 7 . Hata hivyo, Rais ameshikilia  kuwa kafyu ya kutoka saa tatu usiku hadi saa kumi alfajiri itaendelea kuwepo kwa zaidi ya siku 30 zijazo.

Makanisa na misikiti pia itafunguliwa lakini waumini wasiozidi 100 ndio wataruhusiwa kuhudhuria ibada ila kwa muda usiozidi saa moja. Shule za Jumapili na Madrasa kusalia kufungwa kwa muda wa siku 30. Rais pia amesema safari za ndege za humu nchini zitaanza Julai 15, na za kimataifa Agosti mosi.