Posted on: July 14, 2020 Posted by: Kevin Oduor Comments: 0

Awali taarifa katika mitandao ya kijamii imekuwa ikisambaa kuwa shirika la afya ulimweguni (WHO) imetupilia mbali utumiaji wa  barakoa kama njia moja ya kuzuia maambukizi ya virusi vya korona. Vilevile shirika hilo la WHO limesisitiza kuwa kukaa mbali na watu utasambabisha maambukizi ya virusi vya korona na karantini kutupiliwa mbali kwa kuzuia usambazaji wa virusi vya korona.

Kwenye video ambayo imezambaa katika mitandao ya kijami katika mahojiano na kituo kimoja ulimwenguni, Daktari MaryVan Kerkhove ni afisa wa afya wa WHO ambaye alikuwa akidhibitisha madai kuwa kwa sasa kuna watu ambao wanaugua maradhi ya korona na hawawezi kusambaza virusi hivyo kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine.

Van kerhove  alisema maafisa wa serikali bado wanapaswa kupima na kuwatenga watu walioambukizwa , na kumfuatilia mtu yeyote ambaye angeweza kuwasiliana nao. 

Mwezi Juni tarehe saba WHO pia ilirekebisha mwongozo wake kwa  barakoa wiki iliyopita, ikisema inapaswa kuvaliwa katika maeneo ya umma, haswa kwenye usafiri wa umma na katika maeneo yenye watu wengi. Alikubali kwamba utafiti kadhaa umeonyesha kuwa kumekuwa na kusambaa kwa dalili  za mapema katika nyumba za wauguzi.

Daktari MaryVan Kerkhove katika mahojiano yake amedai kuwa Utafiti zaidi na data inahitajika ili kutoa ukweli likiwa virusi vya korona  vinaweza kusambaa sana kupitia  kupitia watu wasioonesha dalili. 

 

Taarifa hii imeendaliwa na Fridah Okachi kutoka chumba cha habari cha Mtaani Radio kwa ushirikiano na shirika la Code For Africa’s iLab data katika programu ya uandishi kwa usaidizi kutoka Deutsche Welle Akademie.