Posted on: July 14, 2020 Posted by: Kevin Oduor Comments: 0

Tovuti ya  runinga ya Citizen Kenya ilichapisha taarifa kuwa  watu watatu walifariki na mmoja kupoteza uwezo wa kuona baada ya kunywa vieuzi.  

Kitengo cha Mtaani Radio cha udhitisho wa habari ghushi kilichunguza uhalali wa taarifa hii. 

Si siri kuwa unywaji wa vieuzi   unasababisha kifo. Afisa wa afya nchini Mexico alidhibitisha kuwa watu  hawa watatu  walikufa na mmoja kupoteza uwezo wa kuona kabisa kutokana na sumu ya methanoli baada ya kunywa vieuzi almaarufu sanitizer.

Wengine  watatu  wako katika hali  mahututi.  Idara ya Afya ya New Mexico ilisema katika taarifa yake kuwa watu wote saba waliaaminika wamelewa sanitizer iliyo na methanoli.

Watu wengine waliripotiwa  kutumia sanitiza ya kunawa mkono  kujilewesha  . Kabla ya janga hilo,  vieuzi  hivyo vilikuwa vimepigwa marufuku katika magereza mengi kulingana na hofu kwamba wafungwa wangeikunywa au kuitumia kuwasha moto. Lakini vituo vya kudhibiti na kuzuia magonjwa vilitangaza kemikali za kutengeneza  vieuzi vinawezatumika  kupambana na viruzi vya korona. 

Kitengo cha Mtaani Radio cha udhitisho wa habari ghushi kimedhibitisha kuwa utuminzi wa vieuzi haswa kama kileo  kinawezasababisha kifo au  madhara kiafya kama vile kuwa kipofu.

Msimaminzi wa afya ya umma  kaunti ya Nairobi  anayehusika na utengenezaji wa dawa Bw Daniel, aneelezea kituo hiki kuwa baadhi ya vieuzi vimezidishwa asilimia sabini ya kileo. Daniel amedokeza kuwa baadhi ya kampuni hapa nchini na duniani hazijaafikia kiwango hitajika na hivyo kampuni kam hizo  huongeza kemikali ambazo hazistahili kwa mwili wa binadamu.

 

Afisa huyo wa afya ya umma hapa jijini Nairobi, amesema kuwa kiwango cha kemikali ya methanol ambayo hupatikana kwa vieuzi ikiwa haijaidhinishwa  inaweza kuwa sumu na kufyonza ngozi. Kiwango kikubwa cha kemikali ya  methanol inaweza kusababisha kichefuchefu, kutapika, maumivu ya kichwa, kuona wazi, upofu wa kudumu, mshtuko, uharibifu wa mfumo wa neva au kifo.

 

Taarifa hii imeendaliwa na Fridah Okachi kutoka chumba cha habari cha Mtaani Radio kwa ushirikiano na shirika la Code For Africa’s iLab data katika programu ya uandishi kwa usaidizi kutoka Deutsche Welle Akademie.