Zaidi ya shule za kibinafsi mia moja nchini Kenya huenda hazitafungua tena hata baada ya janga la Corona kuisha.Hii ni kutokana na madeni ambayo hizi shule zitakua nazo ifikapo mwaka wa 2021 ambapo shule zinatarajiwa kufunguliwa.Baadhi ya shule hizi zipo kwenye mijengo ya kukodiwa,zingine zikiwa zimejengwa kwa mikopo inayohitaji kulipwa.Shule hizi pia hulipa wafanyikazi na walimu wao kutokana na karo walipazo wanafunzi ila kwa wakati huu,wanafunzi wako manyumbani.Hii imeathiri sana wafanyikazi na walimu kutoka shule hizi.Lucy Nyaribo ni mwalimu wa shule moja ya kibinafsi Dagoretti.
Wazazi kutoka shule hizi wanashauku mahali watawapeleka watoto wao kwa kuwa shule za umma zitashuhudia idadi kubwa ya wanafunzi. Watakaoathirika zaidi ni watahiniwa wa mitihani ya kitaifa ambao tayari walikuwa washasajiliwa. Hali hii ilichangiwa pakubwa na mpango wa serikali ya kuhakikisha wanafunzi wote kwa darasa la nane wamejiunga na shule za upili.