Thursday, January 9, 2025
HomeFact checkSIO KWELI: USIMAMINZI WA HUDUMA ZA MJI WA NAIROBI (NMS) HAUSIKI NA...

SIO KWELI: USIMAMINZI WA HUDUMA ZA MJI WA NAIROBI (NMS) HAUSIKI NA UJENZI WA BARABARA YA NGINA DAGORETTI KUSINI

Hisia  mseto zilitawala vinywani mwa wakaazi wa dagoretti kusini kufuatia ujenzi wa barabara ya ngina. Baadhi wakiwa kwenye njia panda kwa kufahamu kuwa  ujenzi huo unaendelezwa na Maja jenerali mohammed mbadi . Na baadhi ya wakaazi wa hapa kaunti ndogo ya dagoreti wakitaja kuwa kutokana na ujenzi unaoendeshwa katika barabara ya ngina road wadi ya waithaka unaendelezwa na mwakilishi wa wadi ya waithaka Antony Kiragu.

kulingana na baadhi ya waliozungumza na mtaani radio kuhusu ujenzi huo wamefurashishwa na ujenzi huo ila kunawale ambao wanashaka ujenzi huo unajengwa na afisi gani ? Je ni afisi ya nairobi metropolitan ama chini ya gavana wa jiji la Nairobi mike sonko?

Kitengo cha kudhibitisha habari ghushi cha mtaani radio kilizungumza na afisi ya ujenzi wa barabara  na imebainika kuwa huduma zinazotolewa na Nairobi metropolitan zipo chini ya kaunti ya Nairobi kwa kuwa afisi ya NMS kuendeleza kazi zake lazima ipokee fedha kutoka idhinisho kutoka kwa afisi ya gavana mike mbuvi sonko.

Katika bango ambacho kimewekwa katika barabara hiyo inaonyesha kuwa ujenzi huo upo chini ya mwakilishi wa wadi ya waithaka antony kiragu na Gavana mike sonko. Hii ikiwa dhihirisho kuwa mwakilishi wa wadi ya waithaka aliweka kipao mbele kujengwa kwa barabara ya Ngina baada ya kufanya mikutano kadhaa na umma.

zaidi na hayo amesema kuwa huenda ujenzi wa barabara hiyo ni mojawapo wa mafanikio chini ya siasa za mwaka wa elfu mbili ishirini na mbili

Taarifa hii imeendaliwa na Fridah Okachi kutoka chumba cha habari cha Mtaani Radio kwa ushirikiano na shirika la Code For Africa’s iLab data katika programu ya uandishi kwa usaidizi kutoka Deutsche Welle Akademie.

 

RELATED ARTICLES

Most Popular

Recent Comments

Solverwp- WordPress Theme and Plugin

Facebook

adapazarı escort Eskişehir escort bayan