Saturday, December 7, 2024
HomeFact checkWAZIRI FRED MATIANG’I HAJALAZWA NA YUPO HOSPITALINI ILIDAIWA.

WAZIRI FRED MATIANG’I HAJALAZWA NA YUPO HOSPITALINI ILIDAIWA.

Uvumi ambao umekuwa ukisambazwa kuwa waziri wa usalama wa ndani Fred Matiang’I anaugua maradhi ya Covid-19

Uvumi umekuwa ukisabazwa katika mitandao ya kijamii haswa katika mtandao wa facebook na twitter kuwa waziri wa usalama wa ndani Fred Matiang’i  amelazwa katika hospitali moja jijini Nairobi almaarufu Agha Khan kwa kuugua maradhi yatokanayo na  virusi vya korona.

Hata hivyo baadhi ya wale waliokuwa wanafuatilia ukurasa wa Kilimani mums and dads uncensored, wengi walionekana kupiga ujumbe huo kutokana kuwa hawajapokea habari yoyote kutoka kwa msemaji wa serikali.

Katika ukurasa mwingine wa kijamii wa  Patrick muriuki ,unaelezea kuwa waziri wa usalama wa ndani fred matiang’i  ni miongoni mwa waziri watatu ambao wanakambiliwa na virusi vya korona . ukurasa huo ukielezea namna waziri wa usalama wa ndani amekosekana katika mikutano ya kutoa taarifa za virusi vya korona kama hapo awali.

Patrick muriuki katika ukurasa huo  akinukuu kuwa habari hizo alizopokea kutoka Daily star ,waziri wa usalama wa ndani alilazwa kutokana na hali yake ya afya kuzoroteka akiwa nyumbani kwake  na hivyo kupelekea kupelekwa hospitali kupata matibabu.

Ukurasa wake Patrick muriuki akinukuu Daily Star , unaaelezea kuwa kutokana na mawaziri watatu kupatikana na virusi vya korona umesababisha kiongozi wa taifa la Kenya Rais Uhuru Kwnyatta akipiga marufuku ya mikutano baina yake na baraza la mawaziri wake.

Kupitia ukurasa wa mtandao wa twitter, katika ukurasa wa wizara ya usalama wa ndani , uliweza kukanusha madai hayo ,waziri Fred Matiang’i hajalazwa.

Taarifa hii imeendaliwa na Fridah Okachi kutoka chumba cha habari cha Mtaani Radio kwa ushirikiano na shirika la Code For Africa’s iLab data katika programu ya uandishi kwa usaidizi kutoka Deutsche Welle Akademie.

 

 

RELATED ARTICLES

Most Popular

Recent Comments

Solverwp- WordPress Theme and Plugin

Facebook

adapazarı escort Eskişehir escort bayan